1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi habari Misri asema wazazi wake wavamiwa na polisi

Amina Mjahid
2 Januari 2020

Mwandishi habari wa Misri maarufu kwa mitizamo yake ya kuikosoa serikali amesema kwamba jana usiku polisi waliivamia nyumba ya wazazi wake na kumtia mbaroni kaka yake.

https://p.dw.com/p/3Vb1e
Ägypten Protest für Pressefreiheit
Picha: picture-alliance/ZUMAPRESS.com/A. Sayed

Mohamed el-Garhy ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter amesema polisi hao waliivamia nyumba ya wazazi wake katika kijiji cha kaskazini mashariki mwa mji wa Cairo na kumuuliza baba yake sehemu alipo mwandishi huyo.

Baada ya baba huyo kuwaambia polisi kwamba mwandishi huyo yuko mjini Cairo walimuamsha kaka yake na kuondoka naye.

El-Garhy ameeleza Twitter kwamba kaka yake Yasser hakuwahi kukamatwa na polisi wala kujihusisha na masuala ya kisiasa. Mpaka sasa kakaake huyo hajulikani aliko wala kama familia hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa polisi kumhusu. 

Katika miezi ya hivi karibuni mamia ya waandishi habari wamekamatwa na serikali ya Misri, na hata kuwafurusha waandishi habari wa kigeni chini humo.

Misri inabakia kuwa mahala pabaya zaidi kwa waandishi habari pamoja na Uturuki na China hii ikiwa ni kulingana na kamati inayowalinda waandishi habari ilioko Marekani.