1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha wa China avuna ushindi wa 'aibu'

15 Aprili 2024

Waandalizi wa mbio za nusu marathon za Beijing wanachunguza video iliyosambazwa mitandaoni inayoonyesha wanariadha watatu wa Kiafrika wakimruhusu He Jie wa China kushinda kimakusudi.

https://p.dw.com/p/4eoCt
 Marathon China
Wanaridha katika mbio za masafa marefu, China.Picha: William West/AFP/Getty Images

Video hiyo ya za mbio za Jumapili ilionyesha Wakenya Robert Keter na Willy Mnangat, Dejene Hailu wa Ethiopia wakimyoshea He eneo la kumaliza mbio hizo na kuonekana wakipunguza kasi ili kumpisha mbele mwanariadha huyo wa China.

He, mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za marathoni za Michezo ya Asia 2023, alishinda mbio hizo kwa saa 1:03:44 sekunde moja mbele ya wanariadha hao wa Afrika.

Tukio hilo limezagaa kwenye mtandao ya kijamii ya China, huku baadhi ya watumiaji wakikosoa ushindi huo na kuutaja kama matokeo ya "aibu".

Kwa mujibu wa afisa mmoja kutoka Ofisi ya Michezo ya Beijing, ambaye alizungumza kwa sharti la kutotajiwa jina amesema uchunguzi unaendelea na matokeo yatatangazwa hadharani.

Bildergalerie China 2015 Leichtathletik-Weltmeisterschaft
Picha: Picture alliance/landov/Xinhua/L. Gang

Mbio za masafa marefu zimeshamiri katika miaka ya hivi karibuni miongoni mwa watu wa tabaka la kati la China, lakini kumekuwa na visa vingi vya udanganyifu na maandalizi duni.

Mnamo mwaka wa 2018, katika mbio za nusu-marathon katika mji wa kusini wa Shenzhen, wanariadha 258 walifanya udangayifu wengi wao wakitumia njia za mkato.