Mwanamke ajitoa mhanga kwa kujilipua nchini Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwanamke ajitoa mhanga kwa kujilipua nchini Pakistan

PESHWAR.Mwanamke mmoja amejitoa mhanga kwa kujilipua mbele ya kituo cha ukaguzi kwenye jimbo la Peshwar.Hata hivyo mbali ya mlipuaji hakuna mtu mwengine aliyekufa.

Inaaminika kuwa hilo ni tukio la kwanza kwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga kuwa mwanamke katika kipindi cha miaka saba iliyopita nchini Pakistan.

Mara ya mwisho kwa mwanamke kuhusika katika harakati hizo ilikuwa mwaka 2000 wakati mwanamke mmoja alipojilipua kwenye ofisi za gazeti la nation jijini Karachi ambapo watu watano waliuawa

Katika shambulizi hilo la jana, Polisi wamesema kuwa mwanamke huyo anahisiwa kuwa ni kutoka Afghanistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com