1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja kabla kufanyika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo

Zainab Aziz Mhariri: Grace Patricia Kabogo
24 Julai 2019

Mwaka mmoja kabla ya kufanyika michezo ya olimpik iya mjini Tokyo, Japan tayari migogoro kadhaa imejitokeza. Baadhi ya viongozi wa kamati ya olimpiki ya kitaifa wanakabiliwa na madai ya ufisadi.

https://p.dw.com/p/3MfjI
Japan Osaka | G20 Gipfel | Thomas Bach und  Yoshiro Mori
Picha: Reuters/K. Kyung-Hoon

Mashindano ya michezo ya olimpiki ya kipindi cha kiangazi yamepangwa kuanza tarehe 24 mwezi julai mwaka ujao mjini Tokyo, Japan. Hadi wakati huo ujenzi unatarajiwa kukamilishwa kwa ajili ya mashindano.

Rais wa kamati hiyo Thomas Bach aliefanya ziara mjini Tokyo mwaka uliopita pia amesifu hatua iliyofikiwa na amesema matayarisho hayo ya mjini Tokyo hayana kifani. Msemaji wa kamati ya maandalizi ya michezo ya Tokyo Masa Takaya ameahidi kwamba mashindano yatakayofanyika katika mji huo yatakuwa kwa ajili ya wote. Amesema pande zote zitanufaika. Bwana Takaya ameeleza kuwa mashindano hayo yatafanikiwa ikiwa lengo hilo litafikiwa. Lakini kauli hiyo inaficha mambo fulani.

Aliyekuwa mjumbe wa kamati ya olimpiki ya kitaifa, hadi mwezi uliopita bwana Tsunekazu Takeda anakabiliwa na tuhuma za ufisadi. Mwendesha mashtaka mkuu wa Ufaransa alianza uchunguzi wa mjumbe huyo miaka mitatu iliyopita. Bwana Takeda ndiye alieongoza timu ya Japan ya kuwania kutayarisha mashindano ya majiji. Anakabiliwa na tuhuma za kutoa hongo ili kununua kura za wajumbe ili mji wa Tokyo uandae mashindano ya michezo ya kiangazi mwaka ujao, 2020.

Pamoja na mgogoro huo, gharama za matayarisho. Kulingana na hesabu za hapo mwanzoni, zilihitajika dola bilioni 6.6. Waandalazi walisema walipa kodi hawatabebeshwa gharama zozote. Lakini baada ya miaka mitatu kamati ya wataalamu iliyoundwa na meya wa jiji la Tokyo imekadiria kwamba kiasi cha dola bilioni 30 kitahitajika kwa ajili ya matayarisho ya mashindano ya mwaka ujao. Ndiyo kusema walipa kodi watabebeshwa mzigo mkubwa wa gharama.

Uwanja mpya unaojengwa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya 2020 mjini Tokyo, Japan
Uwanja mpya unaojengwa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya 2020 mjini Tokyo, JapanPicha: Getty Images/AFP/T. Yamanaka

Gharama hizo zimekadariwa na kamati ya meya wakati ambapo deni  la taifa nchini Japan linavuka asilimia 200  ya  pato jumla la taifa.  Marika yafuatayo ndiyo yatakayoubeba mzigo huo. Hata hivyo msemaji wa kamati ya olimpiki ya nchini Japan bwana Takaya ameeleza kwamba watu wote watanufaika na michezo ya olimpiki na wataona thamani yake. Lakini kwa gharama za kiasi gani. Ameahidi kuwa wafadhili watabeba gharama hizo. Hata hivyo bwana Takaya amesema kwa ajili ya ukarabati wa viwanja fedha za walipa kodi zitahitajika.

Msemamji huyo ameeleza kuwa kazi hiyo ya ukarabati haizingatiwi kuwa gharama, bali ni vitega uchumi vitakavyoleta faida za muda mrefu. Amesema kazi kubwa ya ujenzi itaanza katika sekta ya michezo. Shughuli za ujenzi wa viwanja vya michezo zimegubikwa na kashfa.

Jumuiya ya wafanyakazi ya kimataifa ilichapisha ripoti inayobainisha kwamba wafanyakazi wanatumikishwa kwa muda wa siku 28 bila ya mapumziko na nusu yao wanafanya kazi bila ya mikataba ya maandishi. Watu hao pia wanajinunulia mavazi ya kulinda usalama wao. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wafanyakazi wawili wameshakufa kutokana na mazingira ya hatari ya kazini. Baadhi ya wafanyakazi ni wazee waliostaafu. Wanalazimika kufanya kazi ili kujiongezea mapato kutokana na pensheni zao ndogo.

Mazingira ya kazi pia ni mabaya kutokana na malipo ya chini huku kazi ikiwa ngumu. Mashindano ya michezo ya olimpiki itakapofunguliwa mwaka ujao mjini Tokyo baadhi ya wafanyakazi watakuwa na hasira badala ya furaha, licha ya  kushiriki katika matayarisho.

Chanzo: http://www.dw.com/a-49686068