1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaMarekani

Musk, Zuckerberg kuzungumzia teknolojia ya akili ya bandia

14 Septemba 2023

Baraza la Congress nchini Marekani liliwaalika hapo jana na kufanya mazungumzo na wamiliki wakuu wa makampuni ya teknolojia ili kuelezea mipango na miradi yao inayohusu teknolojia ya akili bandia.

https://p.dw.com/p/4WJHh
Elon Musk und Mark Zuckerberg
Picha: Manu Fernandez, Stephan Savoia/AP Photo/picture alliance

Walioalikwa ni pamoja na Elon Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Tesla na X (Twitter) na Mark Zuckerberg (mmiliki wa Facebook na Instagram).

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya "OpenAI" na mwanzilishi wa teknolojia ya akili bandia ya "ChatGPT" Sam Altman na mwanzilishi wa "Microsoft" Bill Gates walihudhuria pia mkutano huo, ambao vyombo vya habari havikuruhusiwa kushiriki.

Soma pia: Teknolojia ya Akili bandia huenda ikasababisha ubaguzi

Marekani inafanyia kazi sheria mpya zinazolenga kudhibiti teknolojia hiyo, ikifuata nyayo za Bara la Ulaya baada ya mataifa mengi ulimwenguni kuhoji juu ya hatari ya teknojia ya akili bandia ikiwa ni pamoja na kupunguza ajira, kuzagaza habari potofu mtandaoni na athari nyinginezo.