1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni alaani mauaji ya watalii

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amelaani mashambulizi katika mbuga ya wanyama yaliyowaua wanandoa wawili waliokuwa kwenye fungate yao na kuyaita kuwa matendo ya uoga, huku akiapa washambuliaji watalipa kwa maisha yao.

https://p.dw.com/p/4XhB0
Yoweri Musevini to sign anti-LGBT law
Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Museveni amelitaka jeshi la Uganda na vikosi vya usalama vihakikishe makosa haya hayatokei tena na kwamba kundi la ADF linatokomezwa kabisa.

Soma zaidi: Mauaji ya watalii yazusha wasiwasi Uganda

Polisi ya Uganda imesema raia wa Uingereza na mmoja wa Afrika Kusini waliuliwa pamoja na muongozaji safari wao raia wa Uganda katika shambulizi la siku ya Jumanne (Oktoba 17), ambalo linashukiwa kufanywa na waasi wa kundi la ADF wanaoendesha shughuli zao katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma zaidi: Uingereza yatoa tahadhari kwa raia wake Uganda

Watu hao walishambuliwa walipokuwa wakifanya safari katika mbuga ya wanyama ya Malkia Elizabeth kusini magharibi mwa Uganda na gari yao ikatiwa moto.