Museveni akiri maafisa wa usalama kumuua bondia mashuhuri | Matukio ya Afrika | DW | 04.01.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Museveni akiri maafisa wa usalama kumuua bondia mashuhuri

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekiri kuwa askari wa usalama ndiyo waliohusika na mauaji ya bondia mashuhuri nchini humo, hatua ambayo imetajwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kielelezo cha maovu yanayoendelezwa na utawala

Katika hotuba yake ya mwaka mpya kwa taifa, rais Museveni alithibitisha kuwa askari wa vyombo vya usalama ndiyo walitekeleza mauaji ya bondia mashuhuri Isaac Zebra Senyange katika jaribio lao la kutaka kumkamata kuhusiana na madai kuwa alihusika katika kutoa mafunzo kwa makundi ya vijana waliolenga kuvuruga amani wakati wa uchaguzi. Alisema.

Hapo awali polisi walidai kuwa hawakuwa na habari zozote kuhusu waliohusika katika mauaji ya Zebra Senyange na kuahidi kufanya uchunguzi. Lakini baada ya kiongozi wa nchi kujitokeza waziwazi kuhusu kisa hicho, watu mbalimbali wamelezea kuingiwa na hofu na mashaka kuhusu vitendo hivyo zikiwa zimesalia siku 9 tu uchaguzi ufanyike. Wanahoji kwa nini askari hao hawakumkamata mtu waliyemtuhumu na kumsaili kisheria.

Uganda Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa rais Museveni Muhoozi Kainerugaba

Kwa upande wao, viongozi wa kisiasa wameelezea mauaji hayo kuwa kielelezo cha jinsi utawala wa sasa unavyokiuka haki za binadamu kwa kutumia majeshi na vitisho kwa wapinzani.

Bondia huyo ambaye yeye na mke wake ni wakufunzi maarufu wa ndondi nchini alifahamika kuwa mfuasi wa chama cha NRM na kulingana na rais Museveni alikuwa akifanya kazi nzuri kuwarekebisha vijana katika mtaa wake wa Bwaise. Aliwahi kuwa mkufunzi wa Bobi Wine katika ndondi. 

Aidha mgombea huyo ameushtumu utawala kwa kuendelea kuwashikilia korokoroni wasaidizi wake zaidi ya themanini bila kuwahuruhusu kuonana na mawakili wala jamaa zao. Wakati huohuo, malumbano kati ya Bobi Wine na Jenerali Muhoozi Kainerugaba mwanawe rais Museveni kwenye jukwaa la tweeter ndiyo gumzo iliyotawala mwishoni mwa wiki.