1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW :Warusi 10 waungua moto

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpr

Watu 10 wamekufa kutokana na moto uliozuka kwenye nyumba ya wastaafu katika jimbo la Omsk kusini ya Moscow.Shirika la habari la Urusi Tass limetoa taarifa hiyo.

Mkasa huo unafuatia mingine iliyotokea kwenye nyumba za kuwatunzia wastaafu nchini Urusi.

Watu wengine 63 pia walikufa kutokana na moto uliotokea kwenye nyumba ya wazee mnamo mwezi machi.

Na mnamo mwezi wa desemba wanawake 45 waliungua moto na kufa katika kituo cha tiba ya ulevi mjini Moscow.