Moscow. Russia yaweka pingamizi kwa Kosovo.
9 Julai 2007Russia imeonya kuwa haitakubali pendekezo linaloungwa mkono na mataifa ya magharibi lenye lengo la kumaliza mkwamo juu ya hali ya baadaye ya jimbo la Kosovo la Serbia
Juhudi za mataifa ya magharibi kumaliza mkwamo unahusu , kuipatia uhuru Kosovo iwapo muda wa mwisho wa mazungumzo ya kuleta muafaka na Serbia utamalizika.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Russia Sergei Lavrov amesema kuwa nchi yake itaunga mkono tu azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya Kosovo iwapo Serbia pia italiidhinisha. Kosovo imekuwa ikipambana kupata uhuru kutoka Serbia , suala ambalo Serbia inalipinga moja kwa moja. Serbia iko tayari tu kuipatia Kosovo mamlaka ya ndani.