Mnangagwa atuhumu wapinzani kuhusika na mripuko | Matukio ya Afrika | DW | 27.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mnangagwa atuhumu wapinzani kuhusika na mripuko

Rais Mnangagwa alituhumu kundi la wapinzani ndani ya chama tawala kuhusika na mripuko katika mkutano wake

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelituhumu kundi la wapinzani ndani ya chama tawala cha ZANU-PF, lililokuwa likiunga mkono azma ya mke wa rais wa zamani Robert Mugabe, Grace ya kugombea urais, kwa kuhusika na mripuko wa bomu katika mkutano wa hadhara aliohudhuria wiki iliyopita.

Madai haya yametolewa wakati alipofanya mahojiano na shirika la habari la Uingereza, BBC. Hata hivyo, hakumtuhumu moja kwa moja bi. Grace kwa kuhusika na mpango huo, lakini alisema anatarajia kwamba wahusika watamatwa mara moja.

Watu wawili walikufa kufuatia mripuko huo, kwenye uwanja wa Bulawayo, wakati Mnangagwa alipokuwa akiondoka jukwaani baada ya kuwahutubia wafuasi wake. 

 

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com