SiasaCameroon
Mkutano wa WTO wamalizika bila maafikiano
30 Machi 2026
Matangazo
Waziri wa Biashara wa Kameruni, Mbarga Atangana, alisema baada ya siku nne za mkutano huo mjini Yaoundé, wameona muda hautoshi kufikia makubaliano kwenye masuala hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO, Ngozi Okonjo-Iweala, alisema anatumai nchi hizo "zitaweza kuurejesha mkataba wa kusitishwa kwa biashara ya mtandaoni ambao umemalizika muda wake, na kuziwezesha kutoza ushuru wa forodha kwenye utumaji wa kielektroniki kama vile kupakua na kutangaza."
Majadiliano hayo yalikwama baada ya Marekani na Brazil kutafautiana juu ya kuongezwa muda huo kwa miaka miwili mingine.
Hata hivyo, mkurugenzi mkuu huyo wa WTO aliongeza kuwa Marekani na Brazil zilikuwa zinafanya mazungumzo baina yao kuukwamua mkwamo huo.