Mkopo kwa Ugiriki | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 12.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mkopo kwa Ugiriki

Shirika la Fedha Ulimwenguni, IMF na Umoja wa Ulaya uliipa Ugiriki mkopo mkubwa, ili nchi hiyo isifilisike.

Shirika la fedha Ulimwenguni, IMF

Shirika la fedha Ulimwenguni, IMF

Ugiriki inatafakari iwapo kuna uwezekano wa kuongeza muda waliopewa kulipa deni lake kubwa. Waziri wa fedha wa Ugiriki George Papa Constantinou, katika mahojiano na televisheni moja ya kibinafsi nchini Ugiriki, SKAI, alisema hadi kufikia sasa hakuna uamuzi uliofikiwa, lakini iwapo muda huo utarefushwa itakuwa ni zawadi kwa kazi nzuri Ugiriki inafanya kuondokana na deni walilopewa ili nchi hio isifilisike. Mkopo huo kwa ugiriki ulitolewa na Shirika la fedha Ulimwenguni IMF pamoja na Umoja wa Ulaya. Waziri Constantinou aliongeza kuwa Ugiriki haijatoa ombi rasmi kutaka kurefusha muda wa kulipa deni hilo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel tayari ameipinga hatua hiyo, akisema kuongeza muda wa kulipa deni hilo sio suluhisho la kuyatatua matatizo ya Ugiriki. Ingawa Ugiriki inaendeleza mpango wake wa kubana matumizi, wawekezaji bado wana shaka shaka kuhusiana na uwezo wa Ugiriki kukabiliana msukosuko wa kiuchumi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com