1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Mjumbe wa UN nchini Libya ajiuzulu huku akiwalaumu wanasiasa

17 Aprili 2024

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya Abdoulaye Bathily amesema amewasilisha ombi la kujiuzulu kutokana na kile anachosema ni kukosekana kwa dhamira ya kisiasa ya kutafuta amani.

https://p.dw.com/p/4erkG
Mjumbe maalum wa UN nchini Libya Abdoulaye Bathily
Bathily anasema viongozi wa Libya wameyaweka maslahi yao mbele badala ya kutafuta suluhisho la mzozo wa nchi hiyoPicha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya Abdoulaye Bathily amesema amewasilisha ombi la kujiuzulu, akisema shirika hilo la kimataifa haliwezi kufanikiwa kuunga mkono mabadiliko ya kisiasa ya nchi hiyokwa sababu viongozi wake wameyaweka maslahi yao mbele badala ya kutafuta suluhisho.

Soma pia:Makazi ya waziri mkuu wa Libya yashambuliwa

Bathily ambaye ni raia wa Senegal ameyasema hayo katika kikao na waandishi habari baada ya mkutano wa Baraza la Usalama ambapo alielezea hali ilivyo mbaya katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, iliyokumbwa na mzozo na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya muongo mmoja.

Bathily amesema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya - UNSMIL ulifanya juhudi nyingi chini ya uongozi wake katika kipindi cha miezi 18 iliyopita lakini hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na ukosefu wa dhamira ya kisiasa na nia njema kutoka kwa viongozi wa Libya. Ameiita hali hiyo kuwa ya kuhuzunisha kwa sababu idadi kubwa ya watu wa Libya wanataka kuondoka katika fujo hiyo.