1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutana na Cabral aliyepigania uhuru kutoka ukoloni wa Ureno

Yusra Buwayhid
25 Julai 2018

Akiibuka kutoka kundi la wapigania uhuru wa Afrika, Amilcar Cabral ameiongoza Guinee Bissau na Cape Verde kuelekea uhuru kutoka watawala wa kikoloni wa Ureno. Lakini aliuliwa kabla ya kulifikia lengo lake.

https://p.dw.com/p/2tVPY

Amilcar Cabral ameisihi muda gani?

Amezaliwa mwaka 1924 mjini Bafatá , Guine Bissau. Wazee wake walitokea Cape verde. Amekulia Sao Vicente
,Cape verde na kusomea fani ya kilimo mjini Lisbone. Alirejea baadae Guinea Bissau. Aliuliwa january 20 mwaka 1973 mjini Conakry nchini Guinea.

Kwanini Amilcar Cabral alikuwa maarufu?

Akiwa muasisi mwenza wa chama cha waafrika wanaopigania uhuru wa Guine na Cape Verde (PAIGC), mwaka 1956, Amilcar Cabral alichaguliwa akuwa katibu mkuu na kuziunganisha nchi hizo mbili katika mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ureno. Chama cha PAIGC kikaiongoza Guine Bissau hadi uhuru mwaka 1973.Cabral alikuwa mpigania haki za Afrika, alikuwa pia mtaalamu wa kilimo na mtunga mashairi..Hakuwa akikubali kuigiza mitindo ya kigeni ya mapambano ambayo  kwa maoni yake hayambatani na mitindo ya amani ya Guine Bissau.

DW Videostill Projekt African Roots | Amílcar Cabral, Guinea Bissau, Kapverden
Picha: Comic Republic

Amilcar Cabral kavutiwa na nani na amewavutia akina nani?

Amilcar Cabral ameyavutia makundi menegine ya ukombozi katika nchi zinazozungumza kireno barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla. Amechangia katika kuundwa kituo cha-Centro de Estudos Africanos, jumuia ya wanafunzi wa kiafrika wanaozungumza kireno na alikuwa na maingiliano na viongozi mashuhuri  wapigania uhuru wa nchi za Afrika zinazozungumza kireno mfano wa Agostino Neto, Mário Pinto de Andrade, Marceelino dos Santos.

Amilcar Cabral

Matamshi mashuhuri ya Amilcar Cabral:

"Waafrika wanatambua kwamba nyoka hata akijibadilisha ngozi, lakini anabakia kuwa nyoka."

"Hatujawahi  hata mara moja kuwachanganya chungu kimoja "ukoloni wa Ureno na wananchi wa ureno". Mapambano yetu ni dhidi ya ukoloni wa Ureno."

"Atakaetaka kuniumiza atakuwa pamoja nasi, hakuna yeyote atakaekidhuru chama cha PAIGC isipokuwa sisi wenyewe."

Nani kamuuwa Amilcar Cabral?

Amilcar Cabral ameuliwa mjini Conakry na mwanachama wa chama chake mwenyewe anaesemekana kapokea amri kutoka Ureno. Lakini maafungamanio hayo yamezusha eti eti nyingi kuhusu nani hasa anabeba jukumu la kifo cha Cabral. Kuna wanaposema aliyemuuwa Amilcar Cabral anajulikana lakini aliyeamuru auliwe hajulikani.

 

Carla Fernandes and Gwendolin Hilse wamechangia kuandika makala hii. Ni sehemu ya makala maalum za  mfululizo wa "Asili ya Afrika", ushirikiano kati ya shirika la DW na taasisi ya Gerda Henkel.

Mwandishi:Fernandes,Carla/Hamidou Oummilkheir
Mhariri:Yusuf Saumu