Messi hatimaye acheka na wavu | Michezo | DW | 07.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Messi hatimaye acheka na wavu

Barcelona waliwanyeshea Sevilla mabao mane kwa bila uwanjani Camp Nou katika La Liga, huku Lionel Messi akiutilia kikomo ukame wake mdogo wa magoli kwa kufunga bao katika mtanange huo.

Kufunga kwa Messi ni habari njema kwa Messi kuelekea mtananga wa El Clasico utakaopigwa baada ya mechi ijayo ya La Liga.

Barca kwa sasa wanaishikilia nafasi ya pili nyuma ya Real Madrid halafu Atletico Madrid wako katika nafasi ya tatu baada ya kutoka sare ya kutofungana na Real Valladolid.