1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Meli ya Urusi yashambuliwa kwa droni

14 Februari 2024

Meli ya Urusi yasemekana imeshambuliwa kwa ndege za droni kwenye kisiwa cha Crimea kilichotekwa na kufanywa kuwa sehemu ya Urusi mnamo mwaka 2014.

https://p.dw.com/p/4cO4R
Bahari Nyeusi | Manuari ya Urusi
Manuari ya kijeshi ya UrusiPicha: Sedat Suna/epa/dpa/picture alliance

Taarifa hiyo imetolewa na vyombo vya habari vya Ukraine. Vyombo hivyo vya habari vimenukuu chanzo bila ya kutaja jina.

Vyombo hivyo vya habari vimekinukuu chanzo hicho kikisema kuwa meli za kivita za Urusi zimeshambuliwakwenye Bahari Nyeusi. Hata  hivyo Ukraine haijatoa tamko rasmi.

Soma pia:Jeshi la Ukraine laizamisha manowari ya Urusi

Kwa mujibu wa taarifa iliyokaririwa, meli ya kivita ya Urusi, Caesar Kunikov imeharibiwa vibaya na imezama. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema tu kwamba droni sita za Ukraine zilidunguliwa kwenye Bahari ya Nyeusi usiku wa jana.