1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mauzo ya silaha Ulaya yaongezeka kwa vita vya Ukraine

Mohammed Khelef
11 Machi 2024

Biashara ya silaha barani Ulaya imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana, kwa kiasi kikubwa, na vita vya Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4dNIx
Ripoti ya SIPRI
Taasisi ya SIPRI inasema kuwa mauzo ya silaha imeongezeka maradufu barani Ulaya kutokana na vita vya Ukraine.Picha: Staff Sgt. N.B./dpa/picture alliance

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Migogoro (SIPRI) imegundua kuwa ununuzi wa silaha wa mataifa ya Ulaya uliongezeka kwa asilimia 94 kati ya mwaka wa 2019 an 2023 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka wa 2014 hadi 2018.

Takwimu hizo za SIPRI zinahusiana na kiasi cha silaha zilizonunuliwa na sio thamani yake.

Soma zaidi: Ujerumani yabadili msimamo kuhusu mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia

Mnunuzi mkubwa wa silaha barani Ulaya alikuwa ni Ukraine na asilimia 23 ya jumla ya uagizaji wa silaha katika kanda hiyo.

Nchi hiyo imekuwa ikipambana na uvamizi kamili wa jeshi la Urusi kwa miaka miwili.

Katika mwaka wa 2023, Ukraine ndiyo iliyoongoza kwa uagizaji wa silaha kote ulimwenguni.

Hata hivyo, kwa kipindi cha miaka mitano, nchi hiyo ilikuwa katika nafasi ya nne ulimwenguni nyuma ya India, Saudi Arabia na Qatar.