Mauaji yaendelea kushuhudiwa Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mauaji yaendelea kushuhudiwa Mogadishu

-

Afisa mmoja na walinzi wake watatu kutoka kikosi cha usalama wameuwawa hii leo katika shambulio la bomu la kutegwa kando ya barabara kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Hasan Ade ambaye ni naibu kamishna wa wilaya ya Yakshid aliuwawa pamoja walinzi wake baada ya msafara wao kushambuliwa na wanajeshi kadhaa wengine wakajeruhiwa vibaya.Kwa mujibu wa afisa aliyetoa taarifa hizo bomu hilo lilitegwa na magaidi walioko Somalia.Wanamgambo wanaofungamana na mahakama za kiislamu wamekuwa wakiendeleza mashambulio dhidi ya wanajeshi wa serikali ya mpito wanaosaidiwa na wanajeshi wa Ethiopia pamoja na wanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Afrika tangu mwishoni mwa mwaka 2006.mwezi uliopita serikali ya mpito na muungano wa kisiasa wa upinzani walikubaliana nchini Djobouti kusitisha mapigano lakini mapatano hayo yamekataliwa na wenye msimamo mkali kutoka mahakama za kiislamu ambao wanashikilia wanajeshi wa Ethiopia lazima waondoke katika ardhi ya Somalia kabla ya kufanyika mazungumzo ya kweli.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com