1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matangazo ya mchana 05.08.2018

Yusra Buwayhid
5 Agosti 2018

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema anaamini rais wa Colombia Juan Manuel Santos pamoja na waasi wa nchini Venezuela ndio waliopanga jaribio la mauaji dhidi yake lilotokea hapo jana. Maelfu ya watu wameandamana mjini Tel Aviv, Israel hapo jana kupinga sheria mpya inayoitambua nchi hiyo kuwa taifa la Wayahudi. Na, Wizara ya afya ya Kongo yasema Ebola imeshaua watu 33 jimbo la Kivu.

https://p.dw.com/p/32dsI