Mataifa ya G7 yaigeukia Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mataifa ya G7 yaigeukia Afrika

Viongozi wa mataifa saba tajiri duniani wanakutana na viongozi wa mataifa ya Afrika Jumamosi(27.05.2017)siku ya mwisho ya  mkutano wao wa kila mwaka ambao umegubikwa na kutokukubaliana kuhusu mabadiliko ya tabia nchi,

G7-Treffen Sizilien EU President Tusk, Canadian PM Trudeau, German Chancellor Merkel, U.S. President Trump, Italian PM Gentiloni, French President Macron, Japanese PM Abe, Britain’s PM May EU President Jean-Claude Juncker pose in Taormina (Reuters/T. Gentile)

Viongozi wa kundi la G7 katika mkutano mjini Sicily, Italia , May ,2017

Pamoja  na  hali  hiyo  ya  kutokubaliana  kuhusu  mabadiliko  ya  tabia  nchi , lakini umoja umepatikana  katika  kupambana  na  ugaidi.

Rais  wa  Marekani  Donald Trump  aliwaambia  wenzake wa  G7 kutoka  Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani , Italia  na  Japan  siku  ya  Ijumaa  kwamba  bado  hajaamua iwapo kuendelea  na  mkataba  wa  Paris  wa  mabadiliko  ya  tabia  nchi  wa  kudhibiti  utoaji wa  gesi zinazoharibu  mazingira za kaboni.

G7 Treffen in Taormina Sizilien Italien Merkel, Trump (Getty Images/AFP/P. Wojazer)

Rais Donald Trump wa Marekani(kulia) na kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) katika mkutano wa G7 mjini Sicily, Italia

Viongozi  wa  Ulaya  wameeleza kukatishwa  kwao  taama  nje  ya  mkutano  huo  kwa kulazimika  kurejea  suala  ambalo wanaamini  limekwisha  tiwa  saini  na  kukamilika  miaka miwili  iliyopita.

Pia kulikuwa  na  msuguano unaoendelea  kuhusiana  na  biashara  ya  dunia, pamoja  na Trump, ambae  alichaguliwa  kwa  ahdi  ya  kuiweka  Marekani  kwanza, akilaumu makubaliano  ya  kibiashara  na  makundi  ya  nchi  kwamba  yamesababisha nakisi katika biashara  na  Marekani na kudai  kile  alichoeleza  kuwa ni "uwanja uliosawa " wa kushughulikia  masuala  ya  biashara.

Hata  hivyo , viongozi  wa  G7 wamesema  kuna  makubaliano  makubwa  kuhusiana  na masuala  kadhaa yanayobishaniwa  ya  sera  za  mambo  ya  kigeni , ikiwa  ni  pamoja  na Syria , Libya na  Korea  kaskazini.

G7 Gipfel runder Tisch (Getty Images/)

Kikao cha ndani cha kundi la mataifa tajiri duniani G7 mjini Sicily

Taarifa za mitandao ya kijamii

Pia  wameahidi  kuongeza  juhudi  zao  kupambana  na itikali kali  baada  ya mwanamgambo  wa  Kiislamu  kushambulia  kwa  bomu  la  kujitoa  muhanga  katika tamasha  la  muziki  ambapo  watu  22  waliuwawa  kaskazini  mwa  Uingereza siku  ya Jumatatu, na kuyaambia  makampuni  yanayotoa  huduma  ya  internet  na  mitandao  ya kijamii "kuongeza  kwa  kiasi  kikubwa" juhudi  zao za  kuzuwia taarifa za  wenye  itikadi  kali.

"Kitisho cha ugaidi  ni  suala  moja   ambalo  nchi  zetu  zote  zinakikabili na  kwa  sasa  kuliko ilivyokuwa  hapo  kabla  tunapaswa  kuongeza  nguvu  zetu  kukabiliana  na  kitisho  hiki," amesema  waziri  mkuu  wa  Uingereza  Theresa  May , ambaye  alishindwa kuhudhuria kikao  cha  jana  Jumamosi  na  kurejea  nyumbani  siku  moja  mapema  kwasababu ya shambulio  hilo  la  Manchester.

Die Britische Premierministerin Theresa May (Imago/Zumapress/T. Akmen)

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May

Italia  imekuwa  mwenyeji  wa  mkutano  huo  wa  G7  katika  kisiwa  cha  Sicily  kuvuta  hisia kwa  ajili  ya  Afrika na madhila  ya wahamiaji  ambao  wanahatarisha  maisha  yao  kwa idadi  kubwa  kwa  kufanya  safari  hatari  katika  bahari  ya  Mediterania  ili  kutafuta  maisha bora katika  bara  la  Ulaya.

Wahamiaji wazidi  kuingia Ulaya

Zaidi  ya  watu  nusu  milioni  wameingia  nchini  Italia  tangu  mwaka  2014, wakati  watu 1,400 walifikishwa  katika  fukwe na  waokoaji  siku  ya  Ijumaa  pekee.

Viongozi  wa  Tunisia, Kenya, Ethiopia , Niger  na  Nigeria  watajiunga  na majadiliano  leo asubuhi , ambapo  Italia inataka mataifa  hayo  tajiri  kabisa  duniani  kusaidia  bara  hilo kuendeleza  uchumi  wake  katika  juhudi za  kuwashawishi  vijana  wa  Kiafrika  kubakia nyumbani.

Uhuru Kenyatta (Getty Images/A.Shazly )

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anahudhuria kikao cha G7 mjini Sicily , Italia

Viongozi  hao  wanatarajiwa  kutoa taarifa  fupi  ya  pamoja  kuliko  ilivyokuwa  miaka iliyopita, ambapo  mwanadiplomasia  mmoja  wa  Ulaya  alidokeza  kwamba   huenda  ikawa ya  kurasa  sita  tu ikilinganishwa  na  kurasa  32 mwaka  jana.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre

Mhariri: Zainab Aziz

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com