1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya haki Tanzania yalaani matumizi ya nguvu

7 Novemba 2025

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Tanzania yamelaani ripoti zilizoenea za mauaji ya dhidi ya raia, baadhi majumbani mwao, katika ghasia za baada ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/53HDF
Tanzania Namanga 2025 | Waandamanaji
Ghasia za uchaguzi nchini Tanzania mnamo Oktoba 30, 2025Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Katika taarifa ya pamoja na mashirika mengine sita yasiyo ya kiserikali, Kituo cha Sheria na Haki za Kibinadamu (LHRC) kimesema kulikuwa na "matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wasio na silaha.

LHRC pia imesema familia zimeachwa zikiwa na kiwewe, na watoto wameshuhudia ukatili dhidi ya wazazi wao.

Vijana ndio waliolengwa katika ghasia nchini Tanzania

Taarifa hiyo imeendelea kusema vijana hasa ndio waliokuwa walengwa na kwamba mamia ya watu wamekamatwa, wengine wakisalia kizuizini bila dhamana.

Imeonya kuwa kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu bado hakijafichuliwa kikamilifu, ikikosoa kukatizwa kwa mtandao na vikwazo dhidi ya vyombo vya habari.