Marekani yaihimiza Uingereza kutolitambua taifa la Palestina
20 Septemba 2025
Matangazo
Wanasiasa hao wa chama cha Republican akiwemo mbunge wa New York Elise Stefanik na seneta Rick Scott, wameyatumia barua mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Canada na Australia pamoja na washirika wengine muhimu, wakiwataka kupinga juhudi katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa za kuihalalisha na kuitambua Palestina kama dola huru.
Stefanik na Scott wamesema kulitambua taifa la Palestina kunaweka kielelezo cha hatari kwamba vurugu na wala sio diplomasia, ndio njia inayofaa kwa makundi ya kigaidi kama Hamas kufikia malengo yao ya kisiasa.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wa nchi yake kuitambua Palestina kesho Jumapili.