1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza na Palestina kujadiliwa kwenye mkutano wa UN

20 Septemba 2025

Zaidi ya viongozi 140 wa dunia wataelekea mjini New York, Marekani wiki ijayo kwa ajili ya mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, utakaotawaliwa mwaka huu na mustakabali wa Wapalestina na Gaza.

https://p.dw.com/p/50nvy
Marekani, New York 2025 | Uchaguzi wa jaji wa mahakama ya ICJ
Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa MataifaPicha: Manuel Elias/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Kwa kukiuka taratibu, Baraza hilo Kuu jana lilipiga kura ya kumruhusu Abbas kuhutubia mkutano huo kwa njia ya video huku akiwakilishwa katika mkutano huo na balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa.

Maafa ya kibinadamu yanayolikumba eneo la Gaza yatakuwa kipaumbele cha mkutano huo, miaka miwili baada ya kuanza kwa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yaliochochewa na shambulio la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023.

Kuanzia Jumatatu, Saudi Arabia na Ufaransa zitaongoza kwa pamoja mikutano kuhusu suluhu la mataifa mawili ya Israel na Palestina, inayolenga kuona pande hizo mbili zikishirikiana kwa amani.