1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaendeleza juhudi ya kumtafuta rubani wake

4 Aprili 2026

Jeshi la Marekani limeendeleza leo juhudi za kumtafuta rubani wake aliyetoweka baada ya Iran kuidungua ndege ya kivita ya Marekani na wakati huo huo kutoa ahadi ya zawadi kwa yeyote atakayetoa habari kumhusu rubani huyo.

https://p.dw.com/p/5Bek4
Iran 2026 | ndege ya Marekani iliyodunguliwa na Iran
Picha iliyotolewa na Iran inayodai na mabaki ya ndege ya Marekani iliyoidunguwa Aprili 3, 2026Picha: IRIB/Handout/REUTERS

Ndege hiyo ya Marekani, iliyotambuliwa na Iran kuwa F-15E, ilikuwa mojawapo ya ndege mbili zilizoshambuliwa jana Ijumaa, huku rubani mmoja akiokolewa na mwingine kutoweka.

Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kupoteza ndege katika ardhi ya Iran tangu kuanza kwa vita hivyo ambavyo vimeingia sasa wiki yake ya sita, hatua inayoweza kuashiria mabadiliko katika mwwelekeo wa vita hivyo.

Kwengineko shirika la atomiki la Iran limesema shambulizi la anga limelenga karibu na kituo chake cha nyuklia cha Bushehr, na kuua mlinzi mmoja na pia kuharibu jengo lingine la karibu.  Shirika hilo limetangaza hayo kupitia chapisho kwenye mitandao ya kijamii. Hii ni mara ya nne kwa kituo hicho kulengwa wakati wa vita.