1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Marekani wakutana Singapore kujadili usalama

31 Mei 2024

Mawaziri wa ulinzi wa China na Marekani wanakutana ana kwa ana mjini Singapore ambapo suala la Bahari ya China Kusini linatarajaiwa kujadiliwa.

https://p.dw.com/p/4gUEm
Singapore | Mawaziri wa Ulinzi wa Marekani na China
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun katika mkutano baina ya mataifa hayo mjini Singapore, Mei 31, 2024Picha: DoD/Chad J. McNeeley/Handout/REUTERS

Mawaziri hao, Lloyd Austin wa Marekani  na Dong Jun wa China, wanakutana tena baada ya miezi 18 katika mwendelezo wa mdahalo wa Shangri-La juu ya masuala ya usalama.

Austin ameelezea wasiwasi wa nchi yake juu ya harakati za kijeshi za China karibu na kisiwa cha Taiwan. Waziri huyo pia amesisitiza uhuru wa matumizi ya Bahari ya China Kusini.

Kwa upande wake, Dong Jun amemwambia Austin kuwa hatua za Marekani, kwa kiwango kikubwa zimekiuka sera yake ya kuitambua China moja.