1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroTaiwan

China yahitimisha luteka za kijeshi kuizunguka Taiwan

25 Mei 2024

China imekamilisha luteka za kijeshi za siku mbili katika eneo linaloizunguka Taiwan ambayo kwa kiasi kikubwa yamechukuliwa kama jaribio la kukitisha kisiwa hicho kinachojitawala kidemokrasia pamoja na washirika wake.

https://p.dw.com/p/4gHAs
Taiwan | Ndege za kivita za Taiwan chapa F-16 zikipiga doria
Ndege za kivita za Taiwan (chapa F16) zikipiga doria wakati China ilipokuwa ikiendelea na luteka zake za kijeshi karibu na kisiwa hicho.Picha: Taiwan Defence Ministry/Handout/REUTERS

Wizara ya ulinzi za Taiwan imesema ndege 111 za China na manowari za kivita zilihusishwa kwenye mazoezi hayo yaliyopewa jina Joint Sword-2024A.

Msemaji wa Jeshi la Ukombozi la China, PLA Kamandi ya Mashariki Li Xi amesema jana kwamba luteka hizo zilikuwa na lengo la kupima "uwezo wa pamoja wa kunyakua madaraka, mashambulizi ya pamoja na udhibiti wa maeneo muhimu.

Soma pia:China yaonya juu ya vita vya Taiwan baada ya luteka za kijeshi 

Katika miaka ya karibuni, China imekuwa ikizidisha vitendo vya vitisho dhidi ya Taiwan, na haijaondoa uwezekano wa kutumia nguvu kukidhibiti kisiwa hicho, hatua iliyojidhirisha zaidi kutokana na luteka hizo.