1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Marekani kuipatia Ukraine msaada mpya wa dola mil. 225

7 Juni 2024

Marekani imesema itapeleka msaada wa kijeshi wa karibu dola milioni 225 nchini Ukraine katika kifurushi kipya kinachojumuisha risasi.

https://p.dw.com/p/4gky7
Joe Biden akiwa nchini Ufaransa
Rais Joe Biden ameahid kuisaidia Ukraine katika vita vyake na Urusi na kusema kamwe hawataiachaPicha: IMAGO/Bestimage

Msaada huo mpya unatolewa wakati Rais Joe Biden akisisitiza tena kwamba wataendelea kuisaidia Ukraine na kamwe hawataruhusu Urusi kuitisha Ulaya.

Silaha hizo zitakatumiwa na vikosi vya Kyiv kushambulia ndani ya Urusi ili kuulinda mji wake wa Kharkiv unaoshambuliwa vikali na Urusi.

Alitoa hakikisho hilo katika hotuba ya jana Alhamisi mbele ya kaburi la Wamarekani kwenye eneo la Normandy wakati wa kumbukumbu ya miaka 80 ya D-Day.

Marekani hivi karibuni iliipa idhini Ukraine kutumia silaha zake kushambulia ndani ya Urusi na hii leo Biden anatarajiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Paris.