Marekani kujiondoa rasmi makubaliano ya tabia nchi ya Paris | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.11.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Marekani kujiondoa rasmi makubaliano ya tabia nchi ya Paris

Marekani imeanza rasmi mchakato wa kujitoa kutoka katika makubaliano ya Paris ya mazingira, kulingana na waziri wake wa mambo ya kigeni Mike Pompeo.

Rais wa  Marekani Donald Trump  alikuwa  mpinzani  mkubwa  wa makubaliano  hayo  wakati  alipokuwa  anawania  kiti  cha  urais, na utawala  wake  umekuwa  ukifanya  kila  unaloliweza kubadilisha sheria  za  mazingira, ukisema zinazuwia  biashara  na  kutoa  kwa nchi  nyingine  nguvu  ya  ushindani.

Pompeo alielezea  kuhusu kile  alichokiita "mzigo usio wa  haki wa kiuchumi uliowekwa  kwa  wafanyakazi wa  Marekani, biashara, na walipa  kodi, kwa  ahadi za Marekani  zilizotolewa  chini  ya makubaliano  hayo," wakati  akitangaza  kujitoa  huko. Amesema ,"mfano bora  na  wenye  uhalisia" utapendekezwa  na  Marekani kupinga  makubaliano  hayo  ya  dunia.

Kanada, Edmonton: Greta Thunberg vor dem Alberta Legislature Building

Mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg

Makubaliano  ya  mwaka  2015 yalitiwa  saini  na  karibu  nchi  zote, na  kuuweka  utawala  wa  Trump  dhidi  ya  karibu  washirika  wake wote  pamoja  na  washindani  wake  wakuu  kuhusiana  na  suala  la mabadiliko  ya  tabia  nchi. Trump  binafsi  ni  mtu  mwenye  shaka na  mabadiliko  ya  tabia  nchi.

Utawala  wa  Trump rasmi uliuarifu  Umoja  wa  mataifa  hatua  yake hiyo  ya  kujitoa  siku ya Jumatatu, ukianza  mchakato  wa  mwaka mmoja  ambao  utakamilika  siku  moja  baada  ya  uchaguzi  wa  rais wa  Marekani  mwaka  2020.

Msemaji  wa  Umoja  wa  mataifa  alilithibitishia shirika  la  habari  la Ujerumani dpa kuwa  taasisi  hiyo  ya  dunia  imepokea  barua ya Marekani.

Trump  kwa  kawaida  hutumia  hotuba  katika  mikutano  yake  ya kisiasa  kuonesha  mapenzi  yake  kwa  hewa  safi na  maji safi  na salama. "Tuna  hewa  safi  kabisa katika dunia  hapa  Marekani," ni neno  linalojirudia  kila  mara  kutoka  kwa  rais.

Hata  hivyo , uchunguzi  umeonya  kuwa  tangu  mwaka  2016 baadhi ya  aina  ya  uchafuzi  wa  hewa  unaongezeka.

Bildergalerie Indien Smog

Hali ya uchafuzi wa mazingira mjini New Delhi India

Duniani, wanasayansi  kwa  jumla  wana  wasi  wasi  kuwa ongezeko  la  joto  unaosababishwa na  utoaji  wa  gesi  chafu  wa binadamu  utasababisha  hali  mbaya  kwa  maisha  katika  sayari hii.

Ufaransa  wakati  huo  huo  imelalamikia  uamuzi  huo  wa  Marekani kuuarifu  rasmi Umoja  wa  mataifa  kuwa  inajitoa  kutoka  mkataba huo wa  paris. Wakati  hatua  hiyo  ilikuwa  ikitarajiwa ,"tunasikitika na  inaufanya  ushirika  wa  Ufaransa  na  China  kuhusu  mazingira na  bio anuai kuwa  muhimu  zaidi", ofisi  ya  rais  wa  Ufaransa amesema  wakati  rais Emmanuel Macron akiwa  katika  ziara  rasmi nchini  China.

rtre / afpe / dpae

 

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com