Watu hao wamepoteza maisha kwenye mapigano yaliyozuka Magharibi mwa Uganda baina ya majeshi na wanamgambo wanaotaka kujitenga. Polisi wamemkamata Mfalme wa kabila la Wabakonzo Charles Wesley Mumbere.
Wanamgambo wanaaminika kuwa wanamuunga mkono mfalme huyo ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Yoweri Museveni. Msemaji wa polisi Andrew Felix Kaweesi amesema polisi 14 na waasi 41 wameuwawa katika mapigano hayo yaliyotokea jana katika mji wa Kasese. Mapigano hayo yalizuka baada ya waasi kuwashambulia wanajeshi waliokuwa wanafanya doria katika mji huo.