Mapigano yanaendelea Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mapigano yanaendelea Gaza

Hujuma za jeshi la anga la Israel dhidi ya vituo vya Hamas huko Gaza

Ndege za kijeshi za Israel zimeendelea leo kuushambulia mji wa Gaza, ambapo watu wa nne

Wa kundi la Hamas wameripotiwa kuwawa katika mashambulizi hayo.

Mapema leo kambi moja ya kundi la Hamas ilioko

Mashariki mwa mpaka na Israel ilishambuliwa kwa ndege za kivita za Israel na wapiganaji wa nne wa kundi la Hamas wakauwawa

Afisa wa kijeshi wa Israel amekiri shambulio hilo limefanyika dhidi ya ngome mojawapo ya Hamas.

Afisa huyo amesema ngome hio imekua ikitumiwa na wapiganaji wa Hamas kufanya mashambulizi dhidi ya Israel.

Jana vifaru vya Israel viliingia kwenye ufuo wa ukanda wa Gaza ,msemaji wa Israel akisema, ni jeshi dogo ttu liloingia huko likiwa katika Oparesheni za kujilinda.

Baado haijulikani iwapo Israel inataka kuyahama maeneo yote ya Palastina, ila ttu isalie katika maeneo yalioko mipakani na Palastina .

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema msimamo wake, uko pale pale kuzuru mji wa Sderot ulioshambuliwa kwa makombora ya wapiganaji wa Hamas .

Katika mashambulizi haya ya Israel ambayo yamekua yakiendelea dhidi ya kundi la Hamas,

Wa Hamas wanailaumu Israel kwa kushirikiana na kundi la Fatah la Rais Mahmoud Abbas liweze kuchukua eneo linalogombaniwa ambalo jeshi la Israel lilihama miaka miwili iliopita .

Isreal imeyakanusha madai hayo ya Hamas na kusema kua , wao hawahusiki na ugonvi wa ndani baina ya Hamas na kundi la Fatah.

Majengo yaliokua ya kamati kuu ya Hamas katika Gaza sasa yamebakia mabofu ttu, huku mapigano baina ya kundi la Hamas na Fatah leo yakiripotiwa kupungua.

Nayo Malaysia ambayo ndio mwenyekiti wa Jumuia ya nchi 57 za kiislamu, imeitaka Umoja wa Mataifa, iingilie kati mzozo huu wa wapalastina na Israel .

 • Tarehe 18.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHE8
 • Tarehe 18.05.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHE8

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com