Maoni: Siku za mwisho za Trump zimegubikwa na ghasia | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.01.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Maoni: Siku za mwisho za Trump zimegubikwa na ghasia

Donald Trump na washirika wake ni wakulaumiwa kwa kitendo cha wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mjini Washington, na siku za mwisho za utawala wake madarakani haziji karibuni anaandika Ines Pohl.

Mashambulizi ya rais Donald Trump dhidi ya mfumo wa demokrasia yamefikia kilele. Kauli zake alizozitoa mapema Jumatano zimeendeleza dhana ya kushangaza kwamba uchaguzi aliopoteza miezi miwili iliyopita uliporwa kutoka mikononi mwake na kusababishawafuasi wake kufanya jaribio la mapinduzi.

Hapana shaka kwamba Trump anawajibika kikamilifu na tukio hilo na aliwatuma wafuasi wake watiifu, watu walio na nadharia za kuhujumiwa sambamba na magenge ya watu wa mitandaoni kuvamia jengo la bunge. Marekanai kwa vizazi kadha imekuwa nchi ya matumaini linapokuja suala la uhakikisho wa demokrosia na kukamilisha kipindi cha mpito cha kukabidhiana madaraka, lakini Trump ameweka wazi kwa ulimwengu kwamba mfumo wa Marekani pia ungali na udhaifu.

Ines Pohl Kommentarbild App

Mwandishi wa DW Washington Ines Pohl

Ni muhimu kutambua kwamba hili sio tu tatizo alilotengeneza Trump na mtindo wake wa mashambulizi, bali pia wa kulaumiwa ni watu wake wa karibu ambao mara kwa mara wamechukulia matamshi yake kama ya kutiwa chumvi na kujidai mtandaoni. Hiyo inajumuisha maseneta 12 na zaidi ya wanasiasa 100 wa baraza la wawakilishi ambao wamekubali hoja ya kwamba uchaguzi wa mwezi Novemba haukuwa halali, au angalau kushuku matokeo. Hawakufanya lolote kuzuia kuenea kwa habari za uongo na ghasia. Warepublican wamemwangalia mtu asiye na mipaka akidhibiti chama chao na kumwachia aunde serikali ambayo inafanya kazi kwa ajili yake na sio wananchi. 

Wakati ilionekana kama demokrasia inateketezwa katika majengo ya bunge ya Marekani, rais Trump alikuwa ameketi ofisini kwake Ikulu, akifuatilia kupitia televisheni uharibifu alioanzisha. Ilimchukua saa kadha kabla ya kutoa kauli ya kuwataka kwa unyenyekevu wafuasi wake kudumisha amani. Trump amefanya jitihada kidogo kudhibiti hali kwa kuwaeleza wafuasi wake kwamba "anawependa" na anadhani wao ni "watu maalum".

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kukabidhi madaraka, inaonekana Trump anataka kukididimiza chama chake na misingi ya demokrasia. Tayari ameanza kuwashutumu baadhi ya watetezi wake waaminifu kama makamu wa rais Mike Pence. Trump anasisitiza kwamba Mrepublican bora ni yule tu atakayemtetea hadi dakika ya mwisho. Aina hii ya matamashi imepita kwenye vyombo vya habari vya kihafidhina na kwenye mitandao ya kijamii na ndio ilisababisha hali iliyotokea siku ya Jumatano. Ni dhahiri kwamba Trump hana wasiwasi juu ya jamhuri ambayo anasimamia na angependa kuona ikianguka, ikiwa hatokuwa kiongozi wake.

Washington I Sturm gegen U.S. Capitol

Wafuasi wa Trump walipovamia bunge

Polisi wa bunge ambao wana jukumu la kulinda vyumba vyote vya bunge, wanachama wake na mamia ya wafanyakazi ndani ya jengo hilo, walishindwa kutekeleza jukumu lao. Waandamanaji waliingia bila ya kudhibitiwa, wakati walipovamia bunge, kuvunja madirisha na hata kuingia ofisi ya spika wa baraza la wawakilishi Nancy Pelosi. Mapema mwaka jana wakati waandamanaji wa maisha ya mtu mweusi yana umuhimu walipoandamana kote kwenye jiji la Washington, walikabiliwa na mabomu ya kutoa machozi, na rais huyo alitaka waandamanaji wafungwe kwa kutekeleza haki yao ya msingi.

Ni ukweli kwamba hakuna usawa: Kama wewe ni mzungu na unamuunga mkono Trump, basi wewe ni mzalendo, ikiwa sivyo, wewe ni muasi hatari ambaye unahitaji kupigwa mabomu na kufungwa. Tunashuhudia kitendo cha mwisho cha rais ambaye mara kwa mara amechochea vurugu miongoni mwa watu wake kama kiongozi wao. Kipindi cha mpito kutoka kwa Trump kwenda utawala wa Biden hakiwezi kuja hivi karibuni.

Mwandishi: Ines Pohl