1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni wajitokeza Iran kumuaga Rais Ebrahim Raisi

22 Mei 2024

Mamilioni ya waombolezaji walikusanyika mjini Tehran kumswalia na kutoa heshima zao za mwisho kwa rais Ebrahim raisi aliyefariki dunia katika ajali ya helikopta Magharibi mwa Iran.

https://p.dw.com/p/4g9XC
Iran | Mazishi ya Ebrahim Raisi
Waombolezaji wakihudhuria mazishi ya waathirika wa ajali ya helikopta iliyowaua Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian na wengine, mjini Tehran, Iran, Mei 22, 2024.Picha: Majid Asgaripour/WANA/REUTERS

Televisheni ya taifa nchini humo, ilimuonesha kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, akiongoza ibada hiyo mbele ya majeneza ya Raisi na wenzake wanane walioangamia katika ajali hiyo, akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri hiyo ya kiilsamu Hossein Amir-abdollahian.

Waombolezaji waliokusanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha Tehran waliondoka wakibeba majeneza hayo hadi katika uwanja wa uhuru. Rais Ebrahim Raisi atazikwa kesho alhamisi katika mji alikozaliwa wa Mashad karibu na kaburi la  Imam Reza, ambaye ni Imamu wa nane wa dhehebu la kiislamu la kishia.

Tayari viongozi mbali mbali wa dunia kutoka India, Jordan Qatar Kuwait, Afghanistan, Uturuki na Iraq wamefika nchini humo kuhudhuria maziko hayo hapo kesho.