1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia waandamana mjini Tunis kumuunga mkono Rais Kais Said

Sylvia Mwehozi
20 Mei 2024

Mamia ya watu waliandamana mjini Tunis, wakimuunga mkono Rais Kais Said katikati mwa ukosoaji mkubwa wa ndani na nje ya nchi kuhusu wimbi la kuwatia kizuizini waandishi wa habari, wanaharakati na wanasheria.

https://p.dw.com/p/4g3hX
Kais Saied
Rais Kais Said wa tunisiaPicha: ZUMAPRESS.com/picture alliance

Mamia ya watu waliandamana jana katika mji mkuu wa Tunisia wa Tunis, wakimuunga mkono Rais Kais Said katikati mwa ukosoaji mkubwa wa ndani na nje ya nchi kuhusu wimbi la kuwatia kizuizini waandishi wa habari, wanaharakati na wanasheria. Umoja wa Ulaya, Ufaransa naOfisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za binadamu, zilielezea wasiwasi kuhusu kukamatwa huko na msako uliofanywa na polisi katika makao makuu ya chama cha wanasheria mapema mwezi huu. Mawakili wawili ambao ni wakosoaji wakubwa wa rais walitiwa nguvuni.

Mapema mwezi huu, polisi waliwakamata watu 10, wakiwemo waandishi, mawakili na maafisa wa asasi za kiraia, katika kile kilichotajwa na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty Internatinal kuwa ni ukandamizaji. Wiki iliyopita mawakili walifanya mgomo wakisema mmoja wa mawakili aliyekamatwa wakati wa msako aliteswa.