Majeshi ya Uganda kufunza wanajeshi wa Equatorial Guinea | Matukio ya Afrika | DW | 16.02.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Majeshi ya Uganda kufunza wanajeshi wa Equatorial Guinea

Afisa wa jeshi nchini Uganda amesema serikali ya nchi hiyo imepeleka wanajeshi kadhaa nchini Guinea ya  Ikweta chini ya makubaliano ya kuyapa mafunzo majeshi ya taifa hilo la Afrika Magharibi.

Msemaji wa jeshi  Brigedia Richard Karemire  amesema leo kwamba kati ya wanajeshi 100 na 150 wamepelekwa baada ya makubaliano kutiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwanzoni mwa mwaka huu. Amesema serikali ya Guinea ya  Ikweta ina matumaini kwamba kikosi cha mafunzo na uangalizi kutoka Uganda kitafanya kazi kuelekea kiwango  fulani cha utendaji sahihi wa kazi miongoni mwa majeshi ya nchi hiyo. Uganda na Guinea ya Ikweta yenye utajiri mkubwa wa mafuta yanaongozwa na marais wawili walioko madarakani kwa muda mrefu duniani, na wote  wanakabiliwa na madai ya kuwa watawala wa kidikteta. Guinea ya Ikweta ndiko rais wa zamani wa Gambia  yahya Jammeh alikokimbilia kuishi uhamishoni baada ya kuitawala nchi yake kwa muda wa miaka 22.

 

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com