1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Mahakama Pakistan yakubali rufaa ya Khan ya hatia ya ufisadi

1 Aprili 2024

Mahakama nchini Pakistan leo Jumatatu imekubali rufaa ya Waziri Mkuu wa zamani Imran khan pamoja na mkewe, ya kukutwa na hatia ya ufisadi na kusitisha kifungo chake cha miaka kumi na nne jela.

https://p.dw.com/p/4eJqi
Wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Paksitan Imran Khan wakifanya maandamano
Wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Paksitan Imran Khan wakifanya maandamanoPicha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Hayo yamesemwa na chama cha mwanasiasa huyo ambae pia ni nyota wa zamani wa mchezo wa kriketi na kuongeza kwamba Khan na mkewe wataendelea kusalia gerezani baada ya kukabiliwa na hukumu nyingi, ambazo zilimuondolea sifa Khan kushika nafasi yoyote ya uongozi wa umma kwa kipindi cha miaka 10.

Mahakama Kuu mjini Islamabad imesema kwamba, hukumu ya wanandoa hao itaendelea kuahirishwa hadi uamuzi wa mwisho wa kukutwa na hatia ambao utaendeshwa kwa hoja na ushahidi kama ombi kuu baada ya sikukuu ya Eid Juma lijalo.

Soma pia: Mahakama Pakistan yasitisha kifungo cha Khan na mkewe

Khan na chama chake wanasema kesi mahakamani dhidi yake zinalenga kumuweka nje ya ulingo wa kisiasa, kupitia amri ya jeshi la nchi hiyo ambalo lina ushawishi mkubwa, baada ya kutofautiana na majenerali wa kijeshi.

Jeshi linapinga madai hayo.