1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama kuu yalishutumu shirika la kijasusi la Pakistan

Tatu Karema
27 Machi 2024

Majaji sita wa mahakama kuu ya Pakistan wamelishtumu shirika la kijasusi la taifa hilo kwa kuwatisha na kuwashurutisha kwenye kesi zenye umuhimu wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4eAZF
Mahakama ya juu kabisa ya Islamabad, Pakistan
Picha hii inaonyesha mahakama ya juu zaidi nchini Pakistan. Majaji nchini humo wanalishutumu shirika la kijasusi kwa kuwalazimisha kutekeleza matakwa ya kisisaPicha: Anjum Naveed/AP/picture alliance

Taarifa hii ni kulingana na barua iliyoonekana na shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Barua hiyo iliyoandikwa siku ya Jumatatu, imetoa madai mengi yanayojumuisha moja kwamba mnamo Machi 2023, shinikizo kubwa lilitolewa na maafisa hao wa kijasusi dhidi ya majaji hao kuhusiana na kesi iliyokuwa inamkabili waziri mkuu wa zamani aliye gerezani Imran Khan.

Barua hiyo imeendelea kusema kuwa kwa kuhofia usalama wao, majaji hao walitafuta ulinzi zaidi kwenye makazi yao.

Pia inadai kuwa shemeji wa jaji mmoja alitekwa nyara na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa idara hiyo ya kijasusi na kuteswa ili atoe madai ya uongo.