1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Afrika Kusini yakataa rufaa ya familia ya Lungu

17 Septemba 2025

Mahakama moja nchini Afrika Kusini imekataa ombi la kisheria la familia ya rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu kukata rufaa dhidi ya uamuzi kwamba lazima azikwe katika nchi yake.

https://p.dw.com/p/50bHS
Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya kwa njia ya video mnamo Septemba 24,2020
Rais wa zamani wa Zambia, Edgar LunguPicha: UNTV/AP/picture alliance

Jana Jumanne, mahakama hiyo ilithibitisha uamuzi wake na kuizuia familia hiyo kukata rufaa kwa misingi kwamba hakuna matarajio ya mahakama ya juu zaidi kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini.

Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imesema imeridhika kuwa hakuna sababu za msingi za kutoa ruhusa ya rufaa kwa sababu suala hilo lina maelezo makhsusi na matarajio finyu ya kubatilishwa .

Lungu, ambaye aliongoza Zambia kuanzia mwaka 2015-2021, alifariki dunia mwezi Juni katika hospitali moja nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 68.

Familia yake inataka azikwe Afrika Kusini na pia kumzuia rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema kuhudhuria ama pia kuhutubia katika ibada ya mazishi ya serikali.