1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mahakama Uganda yakataa rufaa ya usajili wa kundi la LGBTQ

Iddi Ssessanga
13 Machi 2024

Mahakama nchini Uganda Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya kundi la utetezi wa mashoga kutaka usajili wa serikali, ikisema linakuza shughuli haramu.

https://p.dw.com/p/4dSnn
Uganda l LGBTQ
Mwanamume wa Uganda akiwa ameshikilia bendera ya upindePicha: uncredited/AP/picture-alliance

Majaji wa mahakama ya rufaa walithibitisha hukumu ya nyuma ya mahakama ya juu iliyounga mkono uamuzi wa mamlaka ya serikalili inayohusika na uasjili zaidi ya muongo mmoja uliyopita kukataa kulisajili shirika la Sexual Minorities Uganda, SMUG.

Soma: Mahakama ya Uganda yaanza kusikiliza pingamizi kuhusu sheria kali dhidi ya ushoga

Kasha Nabagesera anapigania haki za mashoga na wasagaji Uganda akiangazia, kutengwa, chuki na vurugu dhidi yao

Waombaji walitaka kusajili jina hilo "kwa malengo ambayo yalikusudiwa kukuza haki za kujiamiana kwa wachache wanaoainishwa kama LGBT," alisema Jaji Catherine Bamugemereire katika huku aliyoisoma kwa niaba ya jopo la majaji watatu.

Jaji Bamugemereire aliongeza kuwa shughuli za LGBTQ ni kinyume cha sheria na zimetangazwa kuwa uhalifu", na hivyo msajili "alitekeleza maamuzi yake kwa kufuata sheria katika kukataa jina hilo katika maslahi ya umma."Raisi ayalaumu mataifa ya Magharibi kuchochea ushoga

Wanaharakati walitaka kuisajili SMUG kama kampuni ili kuiwezesha kufanya kazi kihalali nchini Uganda, ambapo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria.

Kulingana na hati za korti zilizowasilishwa na waanzilishi wa SMUG, kundi hilo linalenga kulinda haki za watu wachache wa jinsia, kuwapa makazi na usalama pale wanaposhambuliwa, na kutoa utetezi wa umma.

Sheria kali dhidi ya ushoga Uganda

lilipitisha mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya ushoga, jambo lililoibua hasira kutoka kwa watetezi wa haki na mataifa ya Magharibi.

Uganda |Bunge| Kampala
Wabunge wa Uganda wakipitisha muswada wa sheria kali dhidi ya mashogaPicha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Sheria hiyo ina vifungu vinavyoufanya "ushoga uliokithiri" kuwa kosa ambalo adhabu yake ni kifona inatoa adhabu kwa mahusiano ya watu wa jinsia moja yenye maelewano hadi kifungo cha maisha jela.

Maafisa wa SMUG wamelaani hukumu hiyo ya mahakama ya rufaa.

"Uamuzi wa mahakama ya rufaa unaimarisha ubaguzi ulioidhinishwa na serikali dhidi ya walio wachache wa kingono, kuathiri haki za kimsingi za kujieleza na kujumuika," Denis Wamala, mmoja wa walalamikaji, alisema kwenye mtandao wa X, zamani Twitter.Benki ya Dunia yaisimamishia Uganda msaada

Alitoa wito kwa Mahakama ya Juu kufanya "mapitio ya haraka" ya uamuzi wa mahakama ya rufaa.