Magazetini:Matamshi ya Trump yawaacha wachunguzi midomo wazi
19 Julai 2018Mhariri wa gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe anazungumzia matamshi ya kutatanisha ya rais wa Marekani Donald Trump katika vyombo vya habari. Mhariri anaandika:
"Kukana matamshi yake pamoja na maelezo ya kichekesho yamewaacha wachunguzi wa masuala ya kisiasa midomo wazi pamoja na wale ambao wanashindwa kuamini kilichotokea wakiduwaa. Si mambo ambayo rais wa Marekani anaweza kudai, kwamba alichosema watu hawajakielewa. Bila shaka mtu anapoangalia, na kusoma kile anachosema, ni lazima atambue kwamba huyu ni msanii tu. Trump habadiliki. Na pia ni vigumu kumuelewa. Jinsi anavyochukulia mambo, inakumbusha mbinu jinsi dunia ya wafanyabiashara inavyofanya, mchezo wa kuvuruga masuala ya kifedha, ambapo mashirika yanayofanya shughuli za kifedha hujaribu kuvuruga, na kuweka mbele maslahi yake, na hatimaye kufikia lengo lake. Siasa na mashirika ya kibiashara ni kitu kimoja, hata kama kuna tofauti kubwa ya utendaji."
Vyombo vya habari vinawawia vigumu pia, kuripoti kwa usahihi kwa wasomaji na wasikilizaji wa taarifa, inapokuja mada kuhusu mkanganyiko unaotokana na matamshi ya Trump. Anaandika hivyo mhariri wa gazeti la Der Neue Tag la mjini Weiden. Mhariri anaadika:
"Waandishi habari maarufu kama wa gazeti la Der Spiegel la mtandaoni Sascha Lobo akiandika makala yake, aliuliza, ni katika mtazamo gani wa mawazo unaweza kutenganisha, na bila kuchuja ujumbe wa viongozi wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia. Kutokana na kubadilika kwao, ili kujiwekea mpaka baina ya maoni na ripoti, ni kazi kubwa mno hasa katika vyombo vya habari halali vya umma."
Kuhusiana na mada juu ya mjadala wa sera za uhamiaji, mhariri wa gazeti la Stuttgarter Nachrichten anaandika:
"Taifa lenye kifungu cha katiba kinachozungumzia kuhusu haki isiyopingika ya haki za binadamu, linapaswa kuchukua hatua. Hata katika wakati wa kuwapokea wahamiaji ambao hawatakiwi, pamoja na wahamiaji ambao ni wahalifu. Ukweli uko wazi, kwamba nchi hizi wanakotoka wahamiaji hawa si nchi ambazo hazina sera za haki za binadamu. Lakini makundi muhimu ya uchunguzi wa haki za binadamu kama Amnesty International ama Human Rights Watch hawajatoa ushahidi, kwamba ukiukaji wa haki za binadamu uko kwa kiwango kikubwa ama mfumo wao hauaminiki katika nchi hizi. Ni muhimu kuheshimu hilo."
Gazeti la Freie Presse la mjini Chemnitz linazungumzia kuhusu malipo wanayopaswa kulipa watazamaji wa televisheni hapa Ujerumani. Mhariri anaandika:
"Pamoja na uamuzi uliotolewa jana na majaji wa mahakama ya katiba vituo vya televisheni cha ARD na ZDF vitakuwa bado katika mbinyo wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na kizalendo, ambavyo hutoa kashfa dhidi yake. Idadi kubwa ya watumiaji wa vyombo hivyo vya habari, ambao hawatumii vyombo hivyo, wanaona ni kitu cha kushangaza, kulazimika kulipa, wakati hawatazami kabisa televisheni hizo. Majaji lakini wanasema, hali itabaki kama zamani. Hata wale ambao hawana televisheni, ni lazima walipe malipo hayo ya televisheni na redio. Hii si haki, anaadika mhariri. Kwa nini kusiwe na chombo ambacho kinaweza kugundua wale watumiaji wa TV kwa mfano za mtandaoni ama vijana wanaotumia kitu kama Netflix kwa mfano vijana."
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Josephat Charo