1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magari yaliotumika yanaathiri mazingira Afrika

Sudi Mnette
26 Oktoba 2020

Mamilioni ya magari yaliyotumika ambayo yanapelekwa katika mataifa yanayoendelea kutoka Ulaya, Marekani na Japan yanachangia kwa kiwango kikubwa uchafuzi wa hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/3kSaV
Senegal Luftverschmutzung in Dakar
Picha: Getty Images/AFP/Seyllou

Katika ripoti yake mpya iliyotolewa Jumatatu (26.10.2020), Shirika lenye dhamana na ustawi wa mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limeonesha magari ambayo yanapelekwa Afrika kama mabasi madogo na mengineyo yanazuia jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Ripoti hii imejikita katika uchambuzi wa kina ambao umefanyika katika mataifa 146.

Mtendaji Mkuu wa UNEP, Inger Andersen aliongeza kwa kusema "kwa miaka kadhaa, mataifa yaliondelea yameongeza kuyapeleka magari yao yaliyotumika kwa mataifa yanayoendelea." Amesema kukosekana kwa viwango bora na udhibiti kumesbababisha mataifa hayo kuwa kama eneo la kutupia magari yenye kuchafua mazingira na yasiyo salama, aliongeza Anderson.

Afrika inapokea magari mengi chakavu

Kenia | Nairobi | Smog | Luftverschmutzung
Magari yaliotumika kutoka nje, katika jiji la NairobiPicha: picture-alliance/AP Photo/S. A. Azim

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mpya, kati ya mwaka 2015 na 2018, takribani magari yaliyotumika milioni 14 yaliweza kusafurusha katika maeneo tofauti ya ulimwengu. Miongoni mwa hayo asilimia 80 yalikwenda katika mataifa yenye kipato cha chini na cha kati, ambpo zaidi ya nusu ya hayo yalipelekwa barani Afrika.

Kutokana na hali hiyo, shirika UNEP limeyashauri mataifa yalioendelea kuacha kusafirisha magari ambayo hayajweza kufanyiwa ukaguzi wa kimazingira na usalama. Ripoti hii mpya imebaindi theluthi mbili ina sera dhaifu katika zenye kudhibiti uingizwaji wa magari katika mataifa yao. Mataifa ya Afrika yanapokea asilimia 40 ya magari chakavu ambayo yanatoka katika mataifa lengwa.

Hatua hiyo inafuatiwa na Ulaya Mashariki, ambako inapokea asilimia 24 ya magari, eneo la Asia ya Pasifiki asilimia 24, Mashariki ya Kati asilimia 12, na Kusini mwa Amerika asilimia 9. Kwa uchunguzi huo wa UNEP, kwa Uhalozi gari nyingi zinasafarishwa kwa bila kuwa na vyeti thabiti.

Magari magari mengi yana umri wa kati ya miaka 16 na 20.

Na yanatajwa kuangukia katika viwango vya chini vya uchafuzi wa mazingira wa Ulaya EURO4. Waziri wa Mazingira wa Uholanzi Stientje van Veldhoven amenukuliwa akisema "Matokeo hayo yanaonesha uhitaji, kuboresha magari ambayo yanasafirisha kwenda katika maeneo mengine kutoka Ulaya." Waziri huyo aliongeza kusema Uholanzi haina uwezo wa kushughulikia tatizo hilo ikiwa peke yake. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, magari chakavu pia yanahatarisha usalama barabarani.

Soma zaidi:Mbinu za kuokoa mazingira zatafutwa Afrika

Mataifa mengi ambayo yana mifumo dhaifu ya ukaguzi wa magari ambayo yametumika ni Malawi, Nigeria, Zimbabwe na Burundi ambako pia ripoti ya UNEP imebaini uwepo wa ongezeko la matukio ya ajali. Lakini  ripoti imeyataja mataifa ya Afrika ambayo yanataratibu nzuri za udhibiti kama Morocco, Algeria, Ivory Coast, Ghana na Mauritius.

Chanzo DPAE