1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maduro na mkewe wafikishwa kizuizini jijini New York

4 Januari 2026

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amefikishwa kizuizini jijini New York usiku wa Jumamosi, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

https://p.dw.com/p/56IW9
USA 2026 | USA 2026 | Picha iliyotolewa na Jeshi la Marekani ya Rais wa Venezuela Nicolás Maduro
Picha iliyotolewa na Jeshi la Marekani ya Rais wa Venezuela Nicolás MaduroPicha: US President Donald Trump's Truth Social Account/Handout/AFP

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro amefikishwa kizuizini jijini New York usiku wa Jumamosi, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, baada ya kushikiliwa na Marekani kufuatia mashambulizi ya ghafla yaliyolenga maeneo kadhaa nchini Venezuela.

Hatua hiyo ya kushtusha ya Marekani inaonyesha jaribio la kipekee la kuondoa uongozi nchini Venezuela baada ya miezi mingi ya Washington kuongeza shinikizo dhidi ya serikali ya kibeberu ya Maduro.

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba Maduro na mke wake, Cilia Flores, walifikishwa Marekani na kupelekwa kwenye kituo cha Metropolitan huko Brooklyn kwa helikopta usiku wa Jumamosi.

Mahakama Kuu ya Venezuela imeagiza Makamu wa Rais Delcy Rodríguez achukue uongozi wa muda wa nchi hiyo.