1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron afanya ziara ya kushutukiza kisiwani New Caledonia

Sylvia Mwehozi
22 Mei 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara ya kushutukiza katika kisiwa cha New Caledonia katika jaribio la kutatua mzozo wa kisiasa, wakati watalii wakianza kuondolewa kutoka kisiwa hicho kilichokumbwa na ghasia.

https://p.dw.com/p/4g7rq
Macron-New Caledonia 2023
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipotembelea New Caledonia 2023Picha: LUDOVIC MARIN/AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara ya kushutukiza katika kisiwa cha New Caledonia katika jaribio la kutatua mzozo wa kisiasa, wakati watalii wakianza kuondolewa kutoka kisiwa hicho kilichokumbwa na ghasia.

Msemaji wa serikali ya Ufaransa Prisca Thevenot alisema kuwa Macron alitarajiwa kuondoka jana jioni katika jitihada za kutuliza hasira juu ya mipango ya serikali yake ya mageuzi ya upigaji kura iliyokataliwa na wenyeji wa kisiwa hicho. Kwanini New Caledonia imekumbwa na ghasia?

Ziara yake inafanyika wakati Australia na New Zealand zikipeleka ndege zake za kijeshi kuwaondoa watalii waliokuwa wamekwama katika mji mkuu wa New Caledonia wa Noumea.

Kisiwa hicho cha kanda ya Pasifiki chenye wakazi wapatao 270,000 kilitumbukia katika machafuko tangu Mei 13, wakati ghasia zilipozuka kuhusu mipango ya kutoa haki ya kupiga kura kwa maelfu ya wakaazi wasio wa asili.