Maalim Seif agusia mwongozo wa ACT-Wazalendo | Matukio ya Afrika | DW | 02.12.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Maalim Seif agusia mwongozo wa ACT-Wazalendo

Chama Cha ACT Wazalendo kimetoa maelekezo ambayo yataendelea kutumika, wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani 2020 nchini Tanzania.

Akitoa maelekezo hayo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Vuga Mjini Unguja, Mshauri Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema wamelazimika kutoa muongozo huo, kutokana na vitendo vinavyofanywa na watu wanaokusudia kuharibu majengo na kushusha bendera za chama hicho katika matawi ya Unguja na Pemba.

Katika hatua nyengine Maalim Seif ameliomba jeshi la polisi kutenda haki katika utendaji wa kazi zake bila ya upendeleo, kwa kuwa linapaswa kuwahudumia wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Akionesha utulivu wa kuongea, Maalim aligusia miaka mitano ya utulivu na amani uliokuwepo chini ya Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ulioasisiwa na yeye mwenyewe pamoja na aliyekuwa Rais wa Zanzibar Amani Karume ambapo alisema waliingia kwenye maridhiano kwa kujali zaidi maslahi ya Zanzibar na wazanzibari kwa ujumla.