1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza kupunguza wanajeshi wake.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HI

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa serikali yake itapunguza idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo walioko Iraq kwa nusu , na kufikia kiasi cha wanajeshi 2,500 ifikapo majira ya machipuko mwakani.

Waziri mkuu aliyasema hayo katika hotuba katika baraza la wawakilishi.

Hii inakuja wiki moja baada ya kuahidi kupunguza idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Iraq hadi wanajeshi 4,500 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Brown ameliambia bunge kuwa maamuzi yote ya mwisho juu ya kuondolewa kwa wanajeshi yatafanywa kwa ushauriano na uongozi wa jeshi la Uingereza nchini Iraq.