London. Labour kuchagua kiongozi mwezi huu. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

London. Labour kuchagua kiongozi mwezi huu.

Upangaji wa uteuzi wa kiongozi atakayechukua nafasi ya Tony Blair kama kiongozi wa chama cha Labour na John Prescott kama naibu wake unaanza leo Jumatatu.

Kwa mujibu wa muda wa kumchagua kiongozi wa chama cha Labour , wagombea wanapaswa kuwasilisha uamuzi wao kabla ya saa saba na nusu kwa saa za Afrika mashariki tarehe 17 Mei.

Kuweza kuchaguliwa wagombea hao wanapaswa kupata saini za asilimia 12.5 ya wabunge wote wa chama cha Labour, ambao ni kiasi cha wabunge 44, mbali na wao wenyewe.

Kampeni za mwanzo kabisa kati ya kampeni 10 rasmi nchini Uingereza zinatarajiwa kufanyika katika eneo la Coventry hapo Mei 20.

Kwa muda wa zaidi ya miaka 10 mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa chama cha Labour ambaye atakuwa moja kwa moja waziri mkuu mpya badala ya Tony Blair, Gordon Brown amekuwa waziri wa fedha. Je katika wadhifa wa waziri mkuu anatarajiwa kuwa na mtazamo gani.

Muda wa mwisho wa kujiunga na chama cha Labour ili kuweza kupiga kura katika kinyang’anyiro hicho ni Juni mosi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com