1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Austin kujadili kitisho cha Iran katika ziara yake Jordan

Amina Mjahid
5 Machi 2023

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin yupo Jordan ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya Mashariki ya Kati itakayomfikisha Israel na Misri kuonesha uugaji mkono wa Marekani kwa washirika wake dhidi ya kitisho cha Iran.

https://p.dw.com/p/4OH9n
Deutschland Ramstein | US-Verteidigungsminister Lloyd Austin
Picha: Michael Probst/AP Photo/picture alliance

Kabla ya kuondoka Marekani, Austin aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, atakutana na viongozi wa maeneo hayo na kuwahakikishia kuwa Marekani inazingatia uthabiti wa kanda hiyo na matakwa ya washirika wake. 

Awali idara ya ulinzi ya Marekani ilisema majadiliano yatatuama katika kitisho Iran kinachojumuisha kuwapa silaha, mafunzo na kuvifadhili vikundi vya wakala, uchokozi wake wa baharini, vitisho vya mtandaoni, mpango wake wa nyuklia pamoja na mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani. 

Atakapofika Israel, Austin atazungumzia wasiwasi wake kuhusu vurugu katika ukingo wa Magharibi zinazoipa wasiwasi Jordan na viongozi wa kiarabu na kujadili pia juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano.