Libya yawakamata wahamiaji 948 | Matukio ya Afrika | DW | 25.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

LIBYA

Libya yawakamata wahamiaji 948

Maafisa nchini Libya wanaarifu kuwa askari wa kikosi cha ulinzi wa pwani wamewakamata wahamiaji 948 na kugundua maiti 10 kutoka mataifa ya Kiafrika waliokuwa kwenye boti katika operesheni kadhaa.

Operesheni hizo zilizoanza tangu wiki iliopita, zinafikisha idadi jumla ya wahamiaji hasa wa Kiafrika wanaojaribu kuvuka bahari kwenda Italia lakini wakarejeshwa Libya kuwa karibu 2,000.

Pwani ya magharibi ya Libya ndio njia kuu ya kuondokea kwa maelfu ya wahamiaji wanaokimbia vita na umaskini na kujaribu kuingia barani Ulaya.

Msemaji wakikosi cha jeshi la majini la Libya, Ayoub Qassem, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa walinzi wa pwani waliwakamata wahamiaji haramu katika makundi tofauti.

Kundi la kwanza lilikuwa na watu 97 na la pili lilikuwa na wahamiaji 361, wakiwa kwenye boti za mipira.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com