1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuhesabu kura baado kunaendelea nchini Kenya

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChT1

NAIROBI:

Kura baado zinahesabiwa nchini Kenya kufuatia uchaguzi wa urais na ubunge wa alhamisi.Ushindani mkali ni kati ya rais Mwai kibaki na mpinzani Raila Odinga .Matokeo rasmi yatatolewa baadae Ijumaa. Wagombea hao wawili kila mmoja ameahidi kuanzisha elimu ya sekendari ya bure. Idadi ya watu waliojitokeza inasemekana kuwa ilikuwa kubwa ambapo mistari mirefu ilionekana katika vituo vya kupigia kura.Wachunguzi zaidi ya elf 15 wametoka umoja wa Ulaya pamoja na mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki kushuhudia uchaguzi huo.