Kremlin yamshtumu Zelensky juu ya Siku ya Ushindi
9 Mei 2026
Matangazo
Kabla ya sherehe hiyo ya leo ya Siku ya Ushindi ya uliokuwa Umoja wa Kisovieti dhidi ya utawala wa Kinazi wa Ujerumani katika Vita vya Pili vya Dunia, msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, ameiambia televisheni ya serikali ya Urusi kwamba hawahitaji ruhusa ya mtu yeyote kuandaa sherehe hizo.
Peskov ametoa onyo kwa yeyote atakayejaribu kudhihaki na kufanya utani kuhusu siku hiyo.
Ameongeza kusema kuwa "Siku ya Ushindi"inaadhimishwa katika sehemu kubwa za uliokuwa Umoja huo wa Kisovieti kama "siku ya fahari na machozi," na kwamba Umoja huo ambao sasa umevunjika na ambao pia uliijumuisha Ukraine, ulipoteza zaidi ya watu milioni 27 wakati wa ukombozi wa Ulaya kutoka kwa dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler.