Klitschko anataka kupigana katika Olimpiki Rio 2016 | Michezo | DW | 28.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Klitschko anataka kupigana katika Olimpiki Rio 2016

Bingwa wa dunia wa ndondi katika uzani wa juu (heavyweight) Vladmir Klitschko wa Ukraine amesema anataka kushiriki katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro mwaka wa 2016.

Shirika la habari la Ukraine, Interfax limemunukuu bondia huyo akisema kuwa anatumai shirikisho la kimataifa la ndondi litamhurumia na kwamba atakuwa na afya nzuri na motisha ya kuzirusha ngumi katika michezo ya Olimpiki miaka miwili ijayo. Klitschko mwenye umri wa miaka 38 alishinda nidhani ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Atlanta mwaka wa 1996.

Bondia huyo anasema alizungumza na kocha wake wa zamani, Emanuel Steward, wakati wa michezo ya Olimpiki jijini London mwaka wa 2012 na akampa motisha ya kumtaka ashuke ulingoni mjini Rio. Steward alifariki mwezi Oktoba mwaka huo.

Klitschko siku ya Jumapili, alihifadhi mikanda yake ya WBO; WBA; IBO na IBF mjini Oberhausen, hapa Ujerumani, katika pigano lake la dunia la 25, kwa kumwangusha sakafuni mpinzani wake Muaustralia Alex Leapai baada ya dakika mbili na sekunde tano za raundi ya tano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman